NEWS

VIDEO: Kutana na kijana Rashid Mkwela, Mtanzania wa kwanza kujenga nyumba ya kisasa kwa kutumia matairi chakavu ya magari, Atumia mamilioni kukamilisha ujenzi

Katika harakati za kutunza mazingira watu wengi wamekuwa wakihaha namna gani wanaweza kutumia takataka au vitu vilivyoisha muda wake kutumika na kuvifanya vitumike upya, Na hii ndio maana kijana Rashid Mkwela ameamua kutumia matairi ya magari yalikwisha tumika na kujengea nyumba ya kisasa.

Rashid Mkwela, 32, amesema kuwa alipata wazo la kujenga nyumba hiyo baada ya kugudua kuwa kuna taka taka nyingi za matairi chakavu, Ambazo hulazimika kuchomwa jambo ambalo linaharibu mazingira zaidi kwa moshi.
Amesema aliona njia mbadala ni kuyatumia matairi hayo kama materials ya ujenzi kwani anaamini akifanya hivyo nyumba itadumu kwa muda mrefu pia gharama za ujenzi haziwezi kuwa kubwa ukilinganisha na nyumba za matofali ya kawaida.
Akielezea nyumba hiyo, Rashid amesema kuwa ametumia matairi 1000 na jumla ya gharama zote hadi mjengo huo kukamilika ametumia Tsh milioni 10 na amedai kuwa bado anaendelea na finishing.
Tags

Related Articles

Back to top button
Close
Close